Saturday, December 17, 2016

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA LEICESTER KUHUSU SCHMEICHEL

GOLIKIPA wa klabu ya Leicester Kasper Schmeichel hatimaye amerejelea mazoezi katika timu yake baada ya kuumia mkono mwezi Novemba.
Huenda akaweza kucheza mechi ya Jumamosi ya ugenini dhidi ya Stoke City.
Schmeichel, 30, aliumia mkono katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya FC Copenhagen tarehe 2 Novemba ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Leicester wameshinda mechi mbili pekee kati ya nane walizocheza ligini na katika michuano ya kombe la ligi tangu wakati huo.
“Kasper alishiriki mazoezi vyema leo,” kocha wa Leicester Claudio Ranieri alisema Alhamisi wakati akiongea na waandishi.
Schmeichel msimu ulipita alichezea Leicester timu yake mechi 38 za ligi na kumaliza mechi 15 kati ya hizo bila kufungwa.


0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI