Wednesday, November 2, 2016

YANGA WAKUBALI KIPIGO CHA PILI MSIMU HUU DHIDI YA MBEYA CITY

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, leo November 2 2016 walishuka katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza dhidi ya wenyeji wao Mbeya City katika mchezo wao wa 13 wa Ligi  Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017.
Yanga wakiwa ugenini huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo chao cha kwanza kutokaStand United cha goli 1-0 September 25 2016, leo November 2 2016 wamekubali kipigo cha pili kutoka kwa Mbeya City wakiwa katika dimba la Sokoine Mbeya.
Mbeya City wamefanikiwa kuifunga Yanga goli 2-1, magoli ambayo yalifungwa naMwasapili dakika ya 6 na Kenny dakika 36 goli ambalo lilichukua muda kidogo refa kufanya maamuzi kutokana na wachezaji wa Yanga kuligomea, Donald Ngoma ndio alifunga goli la kufutia machozi la Yanga dakika 4 za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI