Wednesday, December 9, 2015

WAZIRI MKUU ATAKA ZOEZI LA USAFI LIWE ENDELEVU

IMGS4237
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
IMGS4254
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015.
IMGS4277
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la  Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
IMGS4287
IMGS4343
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  Kulia kwake ni  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki na Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
IMGS4392
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
IMGS4402
Waziri Mkuu,Kassim Majliwa akiwa amezongwa  na wananchi wakati alipokwenda kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam kufanya usafi Desemba 9, 2015.
IMGS4351
Baadhi ya washiriki wa zoezi la usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam wakipiga picha kwa kutumia simu wakati Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alipozunguza nao baada ya kufanya usafi  sokoni hapo  Desemba 9, 2015.
IMGS4433
 Gari alilopanda Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa likitoka kwenye eneo la soko kuu la Kariakoo alikokwenda kushiriki katika kufanya usafi Desemba 9, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
IMGS4437
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la usafi lililofanyika leo nchini kote lisiishie hapo bali liwe endelevu ili Tanzania iwe na taswira nzuri kwa wageni wanaoingia nchini.
Ametoa wito huo leo kwenye soko la Kariakoo wakati akishiriki zoezi la kufanya usafiikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru yasiwepo na badala yake watu wote washiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi wa soko la Kariakoo wafike ofisini kwake Jumatatu ijayo (Desemba 14, 2015) saa 4 asubuhi ili wamueleze wana mikakati gani ya kuboresha utoaji huduma kwenye soko hilo.
“Natambua kuwa siyo sahihi kupanga chini biashara tulizonazo. Nataka hawa viongozi waje wanieleze wana mpango gani endelevu wa kuboresha soko hili,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
Waziri Mkuu ambaye alienda kufanya usafi kwenye soko hilo,  alilazimika kuzungumza na mamia ya wananchi waliofika kushiriki zoezi hilo. Pia alikagua maeneo mbalimbali ya soko hilo hadi shimoni na kusema aneridhika na usafi uliofanyika bali amesisitiza usafi huo uendelezwe.
“Kaulimbiu ya Mheshimiwa Rais Magufuli ya HAPA KAZI TU inatupa ari ya kufanya kazi. Fanyeni kazi. Watanzania mko huru kufanya kazi yoyote lakini cha msingi fuateni taratibu na kanuni. Serikali hii tumamua kuwajali watu wa chini. Tutahakikisha wajasiriamali wadogo, akinamama lishe na wamachinga mnafanya kazi kwa amani na utulivu, ” alisema.
Rais Magufuli aliamua kuitangaza siku ya leo (Desemba 9, 2015) ambayo ni maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru iwe ni siku ya kufanya usafi nchi nzima ili kuepukana na magonjwa mbalimbali na hasa kipindupindu.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
DAR ES SALAAM.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI