Wednesday, December 9, 2015

RONALDO AVUNJA REKODI YAKE NA KUWEKA MPYA

IGxwi
Mchezaji bora wa dunia mwaka 2014 na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (pichani)ameweka rekodi mpya katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA baada ya hapo jana kufunga goli 4 katika mchezo kati ya Real na Malmo.
Magoli ya Ronaldo yalifungwa katika dakika ya 39, 47, 50 na 58 na kufanikiwa kufikisha magoli 11 katika michezo ya makundi rekodi ambayo ilikuwa haijawahi kufikiwa na mchezaji yoyote.
Kabla ya kuweka rekodi hiyo mpya, Ronaldo alikuwa na rekodi ya kufunga goli 9 katika hatua ya makundi kwa msimu wa 2013/2014 rekodi ambayo pia ilikuwa imefikiwa na mchezaji wa Shakhtar Donetsk, Luiz Adriano aliyoiweka mwaka jana.
Baada ya kufikisha magoli hayo Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga 11 katika michezo ya hatua ya makundi akifuatiwa na Luiz Adriano goli 9 na Ruud Van Nistelrooy, Hernan Crespo na Filippo Inzaghi ambao walifunga goli 8 kila mmoja.
Magoli mengine ya Real Madrid katika mchezo huo wa Malmo yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 12, 24, 74 na Mateo Kovacic dakika ya 70.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI