Sunday, November 22, 2015

JAMIE VARDY AFIKIA REKODI YA RUUD VAN NISTELROOY!!!

jamie-vardyJamie Vardy 
Mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, Jamie Vardy (pichani) amefanikiwa kufikia rekodi ya staa wa zamani wa Manchester United, Ruud Van Nistelrooy kwa kufunga goli 10 kwa michezo 10 mfululizo.
Vardy amefikia rekodi hiyo aliyoiweka Van Nistelrooy aliyoiweka mwaka 2003 kwa kufunga michezo 10 mfululizo rekodi ambayo Vardy ameifikia wakati timu yake ya Leicester City ilipokuwa ikipambana na Newcastle United na kuibuka na ushindi wa goli 3 kwa bila.
Mbali na Vardy kufikia rekodi hiyo lakini kamuacha Van Nistelrooy kwa kufunga magoli hayo katika msimu mmoja wakati Van Nistelrooy alifunga magoli hayo kwa misimu miwili.
#Talkfootball.com

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI