Friday, October 30, 2015

WASANII BUNGENI WATIMIZE WALIYOAHIDI - STEREO


Msanii Stereo amewataka wasanii waliofanikiwa kuchaguliwa kuingia Bungeni, wakatimize wajibu wao kwa kuyatekeleza yale waliyoyaahidi kipindi cha kampeni, na si kuyapuuzia baada ya ushindi.
Stereo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, na kueleza kwamba iwapo hawatattekeleza wananchi hawatasita kuacha kuwachagua kipindi kingine.
"Kikubwa ni kwamba wakatimize yale ambayo waliyaahidi, kwa sababu watu wamewapa ridhaa ya kuwaongoza katika majimbo husika, kwa hiyo wito wangu mkubwa sana kwa muheshimiwa mtarajiwa Joseph Haule na Joseph Mbilinyi, wakafanye yale mambo ambayo wameyaahidi watu, kwa sababu vinginevyo utakuwa ni uongo, kama watashindwa kutekeleza kwa makusudi yale ambayo waliwaahidi watu katika majimbo yao, basi nadhani watastahili kabisa kunyimwa kura kwa awamu inayokuja", alisema Stereo.
Pia Stereo amewataka viongozi hapo kutumia juhudi binafsi kutosubiri uamuzi wa serikali kutekeleza baadhi ya mambo ambayo wanahitaji katika majimbo yao, na kutokuwa wabinafsi kwa kutanguliza matakwa yao wenyewe.
"Kimsingi focus, maendeleo ya watu mbele, ustawi wa watu mbele kwanza ndipo wajiangalie wao, ikiwezekana mara nyingine hakuna haja ya kusubiri sana kwamba kuna mfuko wa kitu fulani hapa kutoka serikalini, unaona serikali inachelewa kufanya kitu fulani sehemu fulani na wewe ni mbunge sehemu hiyo na una kinafasi fulani na unaona kuna pesa ipo kwenye akaunti yako toa fanya, usisubiri mpaka serikali ifanye", alimaliza Rapa Stereo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI