Mgombea
urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh
Edward Lowassa amesema hakuna sababu ya wamiliki wa viwanda vya sukari
kuendelea kuwaumiza wakulima na endapo atapata ridhaa ya watanzania
atahakikisha anarudisha kiwanda cha Mtibwa mikononi mwa wananchi na
atasimamia kuhakikisha jasho la wakulima wa miwa halipotei bure.
Mh.Lowassa
akizungumza na umati mkubwa wa wananchi wa mji wa Dumila na Turiani
wilayani Mvomero alikoanzia mikutano yake amesema kwa nafsi yake
anaumizwa na hali ya wakulima wa miwa kukopwa jasho lao bila kulipwa na
endapo atapata ridhaa atahakikisha kilimo kinawainua wakulima na hakuna
sababu ya wakulima wa miwa kushindwa kunufaika na viwanda
vinavyowazunguka huku wawekezaji wakiendeelea kuneemeka na atahakikisha
kiwanda cha Mtibwa kinarudi katika mikono ya wananchi na kufuta ushuru
wa mazao na mifugo.
Katika mkutano wa mjini Morogoro uliofanyika katika viwanja vya Sabasaba Mh Lowassa akizungumza na maelfu kwa maelfu ya wananchi wa mji wa Morogoro wakiwemo waliokesha katika uwanja huo kusubiri kusikia sera za mabadilko ambapo Mh Lowassa amesema akipata ridhaa hatowaangusha wananchi kwakua amedhamiria kuhakikisha nchi anamaliza matabaka ya wenye nacho na wasiokuwa nacho fursa za ajira na kufufua viwanda.
Nae alikuwa waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza na wananchi hao amesema wananchi wamesubiri sana na sasa wanataka mabadikio kutokana na ahadi zisizotekelezeka ikiwemo huduma za elimu na kuwataka wananchi kufanya maamuzi magumu kwa kuchagua Lowassa ili akasimamia rasilimali za nchi zinufaishe wananchi.
Wagombea
ubunge wa jimbo la Mvomero Mh Osward Mlay na mgombea ubunge jimbo la
Morogoro mjini Marcus Albanus wakizungumza kwenye mkutano wamesema
mabadiliko wanayoyataka wananchi ni sasa hivi ni kuondoa kero
zilizoshindikana kwa miaka mingi ikiwemo kero ya maji hospitali kukosa
madawa pamoja na kufufua viwanda 14 vya mji wa Morogoro vilivyokufa
baada ya kupewa wawekezaji hali inayosababsiha wanwake na vijana kukosa
ajira.
Baada ya mchakamchaka uliovunja rekodi ya kuwa na wananchi wengi mjini Morogoro Mh Lowassa kesho anatarajia kuendelea kunadi sera za mabadiliko katika mkoa wa Simuyu.
0 comments:
Post a Comment