BAADA
ya waziri wa mambo ya nje Bernad Membe kuwapa tahadhari waangalizi
wa uchaguzi kutoka nje ya Tanzania kwa kuwataka kuwa makini na taarifa
watakazokuwa wanazitoa naye naibu katibu mkuu wa chama cha democrasia na
maendeleo CHADEMA Mhe. JOHN MNYIKA ameibuka na kupinga kauli hiyo huku
akisema kuwa hivyo vitisho na kamwe waangalizi
hao wazitishwe na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi
yao
Mapema wiki jana Akizungumza na mabalozi kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema
mwezi Oktoba mwaka huu, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,
Bernard Membe aliwataka waangalizi wa kimataifa
kutofungamana na upande wowote ambapo amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo
yenye mamlaka ya kutoa taarifa na kusisitiza iwapo watabaini mapungufu yoyote
wanapaswa kupeleka kwa tume ya uchaguzi baada ya tume kutoa taarifa
Kauli hiyo mnyika
anasema ni mbinu za kuwapunguza nguvu waangalizi hao na kuwafanya washindwe
kupinga magoli ya mkono yatakayokuwa yanafungwa na chama cha mapinduzi katika
uchaguzi huo..
Angalia video hiyo hapo chini mdau:
0 comments:
Post a Comment