Thursday, September 3, 2015

HII NDIO MIJI YA AFRIKA INAYOKADIRIWA KUJA KUWA NA MAMILIONEA WENGI KUFIKIA MWAKA 2020!

Dunia inabadilika sana siku hizi mtu wangu, watu na wawekezaji wengi sana wanaitupia jicho Africa wakiamini hii ndio sehemu pekee iliyobaki yenye uwezo wa kuikomboa dunia ya kesho.
dsm
Dar Es Salaam Tanzania.
Nimekutana na stori moja kwenye mtandao inayosema kufikia mwaka 2020 Africaitakuwa ni miongoni mwa sehemu zitakazokuwa na ongezeko kubwa la Mamilionea wa Kiafrica, hii ni kutokana na utafiti uliofanyika na kuonyesha kama ukuaji wa uchumi na shughuli za kibiashara zikiendelea kukua kutakuwa hakuna haja wa Mamilionea wa Africa kuwekeza pesa zao sehemu nyingine.
JOBURG
Johannesburg South Africa.
Kati ya miji iliyotajwa kuwa na vigezo hivi ni mji wa Lagos wa NigeriaAccra wa Ghana,Johannesburg wa South Africa na Dar es salaam wa Tanzania.
Kufikia mwaka 2012 Dar Es Salaam ilikuwa na idadi ya mamilionea 1,900 na makadirio yanaonyesha kutokana na ukuaji wa uchumi wetu wa Tanzania kufikia mwaka 2020 jiji la Dar es salaam litakuwa na idadi ya mamilionea wasiopungua 3,000!
Lagos Nigeria
Lagos Nigeria
Licha ya miji hii 4 kuwa yenye vigezo vikubwa zaidi nchi zingine za Africa zenye mamilionea wengi ni; mji wa Cairo uliopo EgyptCape Town uliopo South Africa, Kanoulipo Nigeria na Marrakesh uliopo Morroco.
CAIRO
Cairo Egypt.
cape town SA
Cape Town South Africa.
marrakesh morroco
Marrakesh Morroco.
Picha hii hapa chini inaonyesha makadirio ya ongezeko mamilionea Africa kufikia mwaka 2020 kwenye miji mingine ya Africa…
billionea
 PA

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI