Thursday, February 19, 2015

T.I AMFUNGUKIA MPENZI WA ZAMANI WA IGGY AZALEA KUTAKA NUSU YA PESA ZAKE


RAPA T.I. anayepewa hishima ya kumgundua msanii Iggy Azalea amesema mpenzi wa zamani wa Iggy ‘Jefe Wine’ hana haki ya kupata pesa yeyote kutoka kwa Iggy na muziki wake.
T.I. amesema ataacha tatizo la Iggy Azalea lishughulikiwe na wanasheria wake ila haoni sababu ya kijana huyo kupewa pesa za Iggy au kupokea malipo yeyote.
Siku chache nyuma TMZ iliripoti kuwa mpenzi wa zamani wa Iggy Azalea anasema walifunga ndoa mwaka 2008 na anashahidi ambaye ni daktari walioenda kumuona pamoja walivyokuwa mke na mume. Jefe anataka nusu ya pesa za Iggy Azalea.
Mwezi wa kumi mwaka jana Jefe alitaka talaka kutoka kwa Iggy na kusema waliishi kama mume na mke huko Texas toka September 2008.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI