Tuesday, November 18, 2014

SPORTS ARENA YATISHIA KWA UBORA WA VIJIWE VYA KUANGALIZIA WASAKATA KABUMBU NCHINI *PICHAZ*

JIJINI Dar es salaam kumekuwepo na maeneo mengi ambayo watu huingia kucheki soka, na maeneo mengi mara nyingi huwa hayaridhishi kwa viwango vya kumkidhi mteja kwa asilimia nyingi, kwani mteja hushia kung'atwa na mbu, joto kali, harufu mbaya kutokana na mda mwingine kuwa karibu na vyoo na mambo kadha wa kadha.
Kwa kulitambua hilo ndipo Sports Arena wameamua kuintroduce kijiwe hiki kipya kabisaa cha wadau kucheki na kufurahia kabumbu, iwe ni mechi kali za ndani au nje ya nchi. 
Wadau mbali mbali wakiendelea kufurahia soka katika kijiwe kipya cha SPORTS ARENA kilichopo Kariakoo kati ya mtaa wa Likoma na uhuru  jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wadau wakishuhudia kabumbu katika kijiwe kipya cha SPORTS ARENA kilichopo Kariakoo kati ya mtaa wa Likoma na uhuru  jijini Dar es Salaam.
Kama mdau wa soka unakaribishwa sana kushuhudia soka katika kijiwe hiki cha SPORTS ARENA ambacho ni cha kisasa kabisaaaa na unacheki soka huku kiyoyozi kinakupuliza, yaaani Soka la starehe kabisa linaangaliwa hapa.
Picha na Robert Latonga wa

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI