Saturday, November 1, 2014

SHAA AMTAJA MSANII ALIYEWEZESHEA COLLABO NA REDSAN WA KENYA

KATIKA Exclusive interview na msanii Shaa wa Mj Records, amezungumzia kukutanishwa na msanii Redsan ambaye anaaminika kuwa msanii mkubwa sana Kenya na ngumu kumpata kwaajili ya collabo, Shaa anasema
"Ay na Unity Entertainment ndio wamewezesha collabo hii,wametukutanisha na mpaka kwenye siku ya Video walikuwepo na wakajumuika nasi "
Shaa anaendelea kusema kuwa "kwenye interview huko Kenya alishangaza watu kwa kumpata Redsan kwenye wimbo wake kwani ni msanii wa kipekee huko Kenya ambaye ukifanya naye kazi itafungua milango mingi"
Shaa anasema collabo nyingine na Wakenya zinakuja, Octopizzo yupo kwenye list. Hii ndio video yenyewe inaitwa Njoo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI