Friday, November 14, 2014

JIM CARREY ARUDI UPYA NA DUMB DUMBER BAADA YA MIAKA 20 *PICHAZ*

BAADA ya miaka 20 ya filamu ya Dumb Dumber ya muigizaji wa ucheshi nchini Marekani, Jim Carrey, sasa amerudi tena na muendelezo wa filamu hiyo upya mwaka huu ambayo inaelezea maisha yao baada ya miaka hiyo kupita.
Filamu hii inaelezea maisha ya marafiki wawili  Jim Carrey aliecheza kama Lloyd Christmas na Jeff Daniels aliegiza kama  Harry Dune miaka 20 baada ya safari yao ya mwisho katika filamu ya toleo hilo la kwanza lililotoka mwaka 1994.
Nyota huyu wa filamu ya Mask, anasema kuwa kuna waigizaji wengi wazuri, lakini kati ya wachekeshaji 10, wachekeshaji 8 hawawezi kumfanya mtu acheke kitu ambacho kina mshangaza.
Daniel yeye anasema kuwa, ni kama filamu ya kwanza walicheza wiki iliyopita kwani   hawajakuwa kiumri, hakuna hekima vichwani mwao wala busara na hakuna kitu chochote kilichobadilika kwao  katika kipindi cha miaka 20 iliyopita,
Waandaji wenyewe wanasema kuwa,kila mtu atacheka katika filamu kwani imebuniwa kwa viwango vya juu

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI