Friday, November 14, 2014

MSANII KANSIIME "PANADOL YA WANAUME" APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUANIKA MAKALIO KWENYE VIDEO YAKE!!!!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Uganda Kansiime Jemimah maarufu kama -Panadol wa Basajja- amepelekwa rumande baada ya kukanusha mashtaka ya kusambaza picha za uchi kinyume na sheria za nchi.
Msanii huyo wa kike alikamatwa pamoja na mtengezaji wa muziki wake mwezi uliopita kwa kile waziri wa maadili anasema ni kuhusiana na picha za uchi.
Panadol ametoa vibao kadhaa katika mahadhi ya kufoka lakini ule ambao umemletea shida unaitwa Ensolo Yange yaani mnyama wangu.
Katika video ya wimbo huo kuna sehemu ambapo yeye mwimbaji akiwa kama mhusika mkuu anaonekana akivaa chupi ya G-string huku makalio yake yakiwa nje.
Na pia kuonyesha mapaja yake na baadhi ya maneno ya muziki wake yakiwa ni kinyume na sheria.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI