Tuesday, November 18, 2014

BIKIRA YAWEKWA KUWA KIGEZO CHA WANAWAKE KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI *PICHAZ*

Polisi wa kike waelezwa kudhalilishwa kufanyiwa kipimo cha bikira.
SERIKALI ya Indonesia inaelezwa kuruhusu kuwafanyia wanawake wanaotaka kujiunga na Jeshi la Polisi kipimo cha bikira, shirika la Human rights Watch limeeleza.
Shirika hilo uangalizi wa haki za binaadam liliwahoji Polisi wanawake na wanaotaka kujiunga na Jeshi la polisi ambao tayari wamepimwa katika miji sita ya nchini Indonesia, wawili kati yao wamefanyiwa kipimo hicho mwaka huu.
Kipimo cha bikira kimeorodheshwa kuwa moja ya matakwa ya kuingia kwenye Jeshi, tovuti ya polisi imeeleza.
Wanawake waliofanyiwa kipimo hicho wamesema walipata maumivu na kujisikia kudhalilishwa.
Askari wa kike walishapeleka malalamiko kwa ngazi za juu za jeshi la Polisi bila mafanikio.
Afisa wa juu wa Human Rights Watch, Nisha Varia amesema kipimo hicho ni unyanyasaji na kinawadhalilisha wanawake, amewataka polisi mjini Jakarta kufuta kipimo hicho na kukipiga marufuku nchi nzima.
Polisi nao wanasema kuwa hawafanyi kipimo hicho kwa sasa kwa kuwa wamepiga marufuku.
Hata hivyo hakuna ushahidi wa kutosha kuwa Jeshi la Polisi limesitisha kitendo hicho kwa kuwa katika tovuti yake eneo la kazi tangazo la tarehe 5 mwezi Novemba mwaka 2014 imeeleza kuwa wanawake wanaotaka kuwa polisi wanapaswa kujaribiwa kama wana bikira,hivyo basi wanawake wanaotaka kuwa askari wanapaswa kutunza bikira zao.Wanawake walioolewa hawapewi nafasi hiyo.
Mashuhuda wanasema kuwa jaribio la bikira hufanywa katika hospitali zinazoendeshwa na jeshi la Polisi, vidole hutumika katika kubaini kama mwanamke ni bikira au la.
Shirika la Human Rights Watch limesema kipimo hiki hufanywa na Polisi pia nchini Misri, India na Afghanistan.
Mwaka 2010 Brigedia Jenerali, Sigit Sudarmanto alieleza namna alivyotofautiana na wenzake kuhusu kipimo cha bikira kwa wanawake yeye haungi mkono.
Kisa cha kufanywa kwa kipimo hiki dhidi ya wanawake ni madai kuwa hawahitaji wanawake wasio bikira wakiwafananisha na makahaba.
Lakini swali linabaki kuwa je kuna ushahidi wa kisayansi kuwa aliye bikira hufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko asiye bikira, je asiye na bikira hana adabu kuliko aliye nayo?
Sudarmanto amesema baada ya kulumbana kwa muda mrefu iliridhiwa kusitishwa kwa zoezi hilo, hata hivyo inashangaza kuona bado hali ni ileile japo ahadi ya kusitishwa ilitolewa.
Chanzo: BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI