Sophie Dahl amekuwa kiulizwa maswali kuhusu urefu wake na
kimo cha mumewe
Wanaume ambao ni
wafupi kwa kimo mara nyingi wanasifika kuwa waume bora kuliko wanaume warefu.
Pia inaarifiwa huwa
na busara zaidi kufidia kimo chao, amekiri Adam Gopnik, mwanamme mmoja wenye
umbo dogo.
Wiki kadhaa
zilizopita, wana soshologia wawili kutoka Chuo Kikuu cha New York, walichapisha
waraka mrefu ulioangalizia maisha ya watu wafupi.
Utafiti wao ulizua
mjadala mkali kutoka kwa kile kinachoweza kusemekana kuwa jamii ya wanaume
wenye kimo kifupi.
Waandishi wa waraka
huo wa maswala ya kijamii unaashiria kwamba wanaume wenye haiba ya kuvutia mara
nyingi hupendelewa katika maisha yao hivyo wanaripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na zaidi ya mpenzi mmoja.
Hata hivyo, hitimisho
la waraka huo, pindi mtu anapoupitia, unashangaza. Ni kwamba, watu wafupi wana
ndoa za kudumu zaidi.
Rod Stewart na mkewe Penny Lancaster
Wanafanya hayo,
katika mazingira magumu wakiwa katika umri tofauti na kipato tofauti, na
wanayafanya hayo wakiwa na wanawake wafupi ambao wanawaoa, na wakati mwengine
na hata wanawake warefu wanaokutana nao.
Wanaume wafupi wanaoa
kuchelewa, lakini pindi wanapooa, wanadumu katika ndoa kwa muda mrefu, na kwa
kiwango cha sayansi ya kijamii, angalau wanakuwa na furaha.
Kuna sababu
zinazoonyesha kwa nini wanaume wafupi wanadumu kwenye ndoa.
Nazo ni, wanaume
wafupi wanaonyesha kukata tamaa. Wanaume wafupi wanaishi katika ulimwengu wa
wanaume warefu na wanajua kila fursa inayopatikana, ni bora kuidhibiti.
Hali ya kukata tamaa
ndio inayowafanya wanaume wafupi kuwa wanaume bora kwa wake zao. Watafiti hao
pia walisema kuwa wanaume wafupi hukimbilia kufanya kila kitu kuwafurahisha
wapendwa wao wakati wanume warefu hilo haliwajalishi.
Spika wa bunge la waakilishi Uingereza, John Bercow, na
mkewe Sally
Moja wapo ya ufumbuzi
wa ripoti hiyo pia ni kwamba wanaume wafupi wanafanya kazi chache za nyumbani
wanapokuwa kwenye ndoa kuliko wanaume warefu, ingawa utafiti pia unaonyesha kwa
wanaume wenye kimo kirefu, aina ya kazi zao za nyumbani inatofautiana.
Kwa maana nyengine,
wanaume wafupi hawafiki juu ya makabati. Wanaume wafupi hawadumu kwenye ndoa
kwa sababu ya kutaka kuridhisha, bali wanadumu kwenye ndoa kwa sababu wanataka
kuonekana.
Utafitio huu kama
ulivyosoma hapo awali umeua mjadala mkali lakini pindi mtu anaposoma utafiti
wao kinachojitokeza zaidi ni kuwa wanaume wafupi wanakuwa na ndoa za kudumu.
Hii ni licha ya
mazingira magumu wanayokabiliwa nayo katika ndoa zao na hufanya hivyo na wake
wafupi waliowaoa lakini pia na wanawake warefu wanaokuwa wamewaoa.
Utafiti huo
unahitimika kwa kusema wanaume wafupi hawana kasi ya kuoa lakini wanapooa wao
hudumu katika ndoa zao.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment