Wednesday, October 22, 2014

WAKATI JWTZ IKIMPA WAKATI MGUMU DIAMOND JOKATE KIDOTI AMSAPOTI PLATNUMZ



WAKATI akiandamwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuvaa sare za jeshi hilo bila ruhusa maalumu, msanii wa muziki wa kipya nchini, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond amepigiwa chapuo na mtangazaji wa kituo cha Channel O, Jokate Mwegelo.

Mwegelo amewataka Watanzania kumpigia kura Diamond katika shindano la tuzo ya video bora Afrika inayofanyika nchini Afrika Kusini.
Alisema Watanzania wanatakiwa kuweka uzalendo mbele kwa kumpigia kura msanii huyo kwani ushindi wake utaisaidia Tanzania kuzidi kujulikana kimataifa katika sekta ya muziki na hata katika masuala mengine ya utamaduni.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI