Vita ya Ubunge yaingiza kashfa kwa Miss Tanzania
MISS
Tanzania 2014 na baba yake, Abbas MtemvuWAKATI mtoto wa mbunge wa
Temeke, Sitti Mtemvu akiandamwa na kashfa ya kughushi umri baada ya
kushinda Miss Tanzania 2014, baba mzazi wa mrembo huyo, Abbas Mtemvu,
ameibuka na kudai sakata hilo ni vita ya kisiasa inayoratibiwa na
wapinzani wake ndani ya CCM.
Tangu
Sitti atangazwe mshindi Miss Tanzania katika shindano lililofanyika
Oktoba 11 katika ukumbi wa Mlimani City, wadau mbalimbali wa urembo
wamekuwa wakipinga ushindi wake wakidai hakustahili kutokana na kukosa
sifa ikiwamo ya kutokuwa na umri stahiki.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa Vicoba kwenye klabu ya Jogging ya
Temeke A jijini Dar es Salaam, Mtemvu alisema inasikitisha watu
wanaolitaka jimbo hilo kumwandama kwa kashfa binti yake kwa maslahi yao
binafsi ya kisiasa.
Mbunge
huyo, alisema kama mtu anataka jimbo hilo aende kwa hoja na sio kwa
majungu na kubainisha kwamba, yeye alichaguliwa na wana- Temeke, hivyo
anayelitaka jimbo hilo aende kwa hoja kwa wananchi na si kupakana
matope.
“Sikilizeni…hili
jambo lisifanywe kisiasa, yule binti wanamdhalilisha sana, inasikitika
mtu anaratibu majungu, tena ni matusi makubwa. Sitti wanamchafua tena
wanamwambia kuwa binti niliyemzaa mimi eti mtoto wake, ambaye ni Tamia Abbas Mtemvu…haya ni matusi, kisa siasa,” alisema Mtemvu na kuongeza.
Wanapita
wanasema Mtemvu kahonga milioni 62 za jimbo, jamani hivi fedha za mfuko
wa jimbo zinatoka kwa namna hiyo, haya yote ni…MNEC (mjumbe wa NEC),
kama utaka jimbo njoo kwa hoja si majungu na kuchafuana.
“Kwanza
kwa taarifa yenu mimi sikuja hapa nikitokea mtaani, nilitoka kwenye kazi
yangu, mimi nilikuwa DC (Mkuu wa Wilaya) tena faili langu hadi leo
linaonyesha niko likizo…embu waambieni hao, kwanza nani kwaambia watu wa
Temeke hatuna hela,” alisema Mtemvu huku akishangiliwa na baadhi ya
wana kikundi hicho.
Licha ya
kutomtaja mlengwa lakini wachambuzi wa siasa za Temeke walisema kuwa
kauli hiyo ilielekezwa kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC),
Phares Magesa, ambaye inadaiwa kuwa ameonesha nia ya kugombea ubunge
jimboni humo mwakani.
Magessa,
kwa nyakati tofauti amekuwa akishiriki matukio mbalimbali ya kuimarisha
chama hicho Wilaya ya Temeke, huku akitoa misaada mbalimbali kwa makundi
ya kijamii ikiwamo vikundi vya Jogging na wasanii.
Misaada
ya hivi karibuni ni pamoja na kuchangia mradi wa maji mtaa wa
Tambukareli na Oktoba 24, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi
wa Jamvi la Katiba.
Alipotafutwa
kuzungumzia tuhuma hizo, Magesa alisema hakuna ukweli wowote na kwamba
hawezi kutumia u-NEC wake kumchafua kiongozi yeyote wa chama chake.
“Mimi
kazi yangu ni kuhakikisha wabunge wangu yeye (Mtemvu) na Ndugulile
wanatekeleza vema ilani ya chama chetu ili ukifika wakati wa uchaguzi
tukainadi kwa wananchi, hivyo siwezi kumhujumu,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment