Saturday, October 25, 2014

UNAAMBIWA HAWA NDIO WASANII WA KIZAZI KIPYA WANAOSHINDANA KUVAA NUSU UCH* *PICHAZ*

Na Musa Mateja
KATIKA hali ya kushangaza, mastaa wa kike wa muziki, Esterlina Sanga ‘Linah’ na mwenzake Sarah Kaisi ‘Shaa’ waliibua gumzo kufuatia kuchuana kwa kupozi kihasara mbele ya kamera.
Staa wa muziki wa kizazi kipya Esterlina Sanga ‘Linah’.
Ilikuwa ndani ya Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar kulikokuwa na Tamasha la Fiesta ambapo paparazi wetu alipokuwa ‘back stage’ na kutaka kuwapiga picha, kila mmoja alijiachia na kuonesha mapaja yake kana kwamba walikuwa wakishindana kuonesha nani anayo mazuri.
Staa wa muziki wa kizazi kipya Sarah Kaisi ‘Shaa’.
Hata hivyo, hakuna aliyekuwa tayari kuzungumzia namna alivyovaa ila mara nyingi Linah amekuwa akisema, yeye kama msanii haoni hatari kuvaa hivyo.
Chanzo: GP

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI