KIUNGO
mchezeshaji wa Yanga Myarwanda, Haruna Niyonzima, ameamua kuvunja ukimya
na kusema anasumbuliwa au hajaukamata vizuri mfumo wa kocha mpya,
Marcio Maximo.
Niyonzima alishindwa kuonyesha kiwango cha juu katika mechi iliyopita, Yanga ilipowavaa watani wake Simba.
Niyonzima
raia wa Rwanda amesema kuwa mfumo wa uchezaji anaoutumia kocha wake
ndiyo umesababisha yeye acheze chini ya kiwango na siyo kitu kingine.
Niyonzima
alisema, mfumo anaoutumia kocha wake huyo wa kufanya mashambulizi ya
kushtukiza ‘Counter Attack’ yeye hauwezi tofauti na wachezaji wenzake.
Myarwanda
huyo alisema, yeye hawezi kucheza mfumo huo, mwenyewe amezoea soka la
pasi, akiamini ndiyo linalomfanya aonekane bora katika mechi zao za Ligi
Kuu Bara na mashindano mengine.
“Mashabiki
ujue walikuwa hawajanigundua, mimi kucheza chini ya kiwango siyo kwenye
mechi dhidi ya Simba, mechi nyingi nimekuwa sionekani kutokana na mfumo
anaoutumia kocha wetu.
“Kocha
anataka tucheze mipira mirefu ya kushambulia kwa kushtukiza kwenye lango
la timu pinzani, ambao kwangu ni mgumu, kiukweli siuwezi kabisa, mimi
ninataka tucheze mpira wa pasi nyingi.
“Ninaamini
tukiendelea kuutumia mfumo huo, basi nitaonekana kiwango kushuka kadiri
ya siku zitakavyokwenda, ili nionekane bora tucheze soka la pasi lakini
hivi nitapotea,”alisema Niyonzima ambaye amekuwa akianza michezo yote
ya Yanga msimu huu.
0 comments:
Post a Comment