Kaimu
Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka
Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza akiwaeleza waandishi wa (hawapo
pichani) mikakati iliyoweka iliyowekwa na Mahakama ya Tanzania ili
kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote na kwa wakati kwa vitendo,
kwa kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa mahakamani, wakati wa
mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa
Mahakama ya Tanzania Bi. Mary Gwera.
Picha na Hassan silayo-maelezo
Na Georgina Misama-MAELEZO.
Mahakama
ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote ili
kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri na rufaa kukaa Mahakamani kwa
muda mrefu.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi Mary Gwera wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Akizitaja
hatua zilizochukuliwa na Mahakama Bi Mary alisema, kuboresha bajeti ya
kushughulikia mashauri kupitia mfuko wa mahakama toka bilioni 57 kwa
mwaka 2012/13 mpaka bilioni 88 mwaka 2014/15, Idadi ya vikao vya
Mahakama ya Rufani vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2012 hadi 34 mwaka
2013/14.
Aidha, Bi
Mary alisema kuwa hatua nyingine ni pamoja na kuanzisha kitengo cha
Mahakama Kuu Dar es Salaam kitakachoshughulikia masuala ya utatuzi wa
mashauri kwa njia ya suluhu muafaka, pia uundwaji wa kamati ya kanuni za
Mahakama itakayosaidia kutunga au kurekebisha kanuni ili kuhakikisha
kuwa kanuni zinazotumika Mahakamani si chanzo cha kuchelewa mashauri
Mahakamami.
Naye,
Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri
kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza alisema kuwa Mahakama
imeanza kuchukua hatua za kuimarisha ukaguzi wa shughuli za Mahakama na
maadili ya watumishi kwa kuanzisha kurugenzi ya ukaguzi na maadili.
Aidha, Bw
Kahyoza alivitaja viwango ambavyo kila hakimu au Jaji anatakiwa
kuvitimiza kwa mwaka na muda ambao mashauri yanatakiwa kuwa Mahakamani
kuwa ni Mh. Jaji wa Mahakama Kuu analenga kumaliza kesi 220, Mahakimu wa
Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi kesi 250 na Mahakimu wa Mahakama za
mwanzo kesi 260.
Mahakama
Kuu inatoa rai kwa Watanzania kufika Mahakamani kwa Tarehe zinazopangwa
ili kuisaidia Mahakama kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa
Mahakamani.
0 comments:
Post a Comment