Habari ambazo
zimeandikwa leo mpaka magazetini ni kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Sitti
kuvuliwa taji la Miss Tanzania 2014 huku issue ya umri wake ikiwa moja ya point
kuu za kumvua taji hilo. Inadaiwa pia kuwa kwasasa wajumbe wa kamati ya Miss
Tanzania wamegawanyika ambapo kuna wasioukubali ushindi wa Sitti huku wengine
wakiona sawa tu.
Habari zaidi
zinadai kuwa kamati na waandaaji wa Miss Tanzania wanataka kumvua Sitti taji
ili kuendelea kuweka taswira, imani na usafi wa shindano hilo kwa kuondoa
kashfa ya upendeleo na rushwa kama ilivyo midomoni mwa watu kuhusu shindano
hilo kwasasa baada ya Sitti kukataliwa kuwa Miss Tanzania 2014.
Pia inadaiwa
kuwa kamati ya Miss Tanzania ina hou na issue ya Sitti kufika kwa waandaaji wa
Miss World na hivyo kuweza kulizuia shindano la Miss Tanzania miaka kadhaa au
kufuta ushiriki wao kabisa.
Inadaiwa kuwa ikiwa
Sitti atavuliwa taji basi kuna uwezekano mkubwa Jihan Dimmachk akaiwakilisha
Tanzania katika shindano la Miss World 2015 kutokana na watanzania wengi
kumkubali na kudai ameonewa kuliko hata mshindi wa pili Lilian Kamazima.
Vigezo
vinavyolalamikiwa kumpa ushindi Sitti ni utata wa umri wake huku wazazi
wake mama akisema mwanae ana miaka 29 wakati baba mzazi na Sitti mwenyewe
wakisema ana mika 18 huku passport yake ikionyesha ana miaka 25, umbo lake
anadaiwa kuwa mnene hivyo kukosa sifa za umiss, anadaiwa kuwa na mtoto wa miaka
6-8, swali hakujibu vizuri huku akichanganya na lugha ya kifaransa ambayo awali
hakuichagua, inadaiwa kuwa sifa zake hazikumzidi Jihan na Lilian Kmazima
walioshika nafasi za pili na tatu.
0 comments:
Post a Comment