Je ni sawa kwa kampuni hizi za kitekonoljia kuwa na sera
kama hii?
WANAWAKE wanaofanya kazi na kampuni za Facebook na Apple
wanapewa nafasi ya kipekee katika kazi yao:
Wanapewa fursa ya kugandisha Mayai
yao ya uzazi hadi watakapokuwa tayari kushika mimba.
Facebook imekuwa ikitoa huduma hii kwa wafanyakazi wake
wanawake nchini Marekani tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Sera hii inalenga kuwavutia wanawake kufanya kazi na
Facebook na pia kwa Facebook kupata wafanyakazi wazuri wenye kipaji na
kuwasaidia kuchagua kati ya kazi na uzazi.
Nayo kampuni ya Apple inajiandaa kuanzisha sera hii
ifikapo Januari mwaka 2015.
"tunaendelea kuwapa faida nyingi wanawake , kwa
kuwaongeza muda wa kupumzika baada ya kujifungua, pamoja na kuhifadhi mayai yao
kama sehemu ya mpango wa kuwasaidia baadaye ikiwa watakosa kushika mimba, ''
ilisema taarifa ya kampuni ya Apple.
Kampuni hizo mbili, zinatoa hadi dola elfu 20 kwa
wafanyakazi wanawake kuhifadhi mayai yao na kuyangadisha wakitarajia kuyatumia
wakati watakapokuwa tayari kuzaa au ikiwa watapwa na tatizo la kushika mimba
basi wataweza kuyatumia.
Kuna ushindani mkubwa sana katika kuwaajiri wafanyakazi
wenye talanta na kipawa pamoja na tajriba ya kazi na kampuni hizi pia zinataka
kupata wafanyakazi bora wenye uzoefu wa kazi na watakaofanya kazi na kampuni
hizo kwa mda mrefu.
Baadhi ya wadadisi wanasema jambo la kuhifadhi Mayai ya
wanawake, linawapa uwezo zaidi wa kudhibiti kizazi hata hivyo kampuni hizi
zinapaswa kuwa tayari kuwasaidia wanawake wanaoamua kupata watoto wakiwa
wanafanya kazi badala ya kufanya jambo hili.
Tayari sera hii imekosolewa baadhi ya wanwake wakisema
kampuni hizi zinajali zaidi faida badala ya kuabdilisha mazingira ya kazi na
kufanya mambo kuwa mepesi kwa wanawake wanaofanya kazi nao.
Kwa kuwa wanawake wengine huwa hawako tayari kushika
mimba, kwa sababu labda ya maujukumu ya kikazi na kazi nyingi, wao hauamua
kuhifadhi mayao ya o kwa mnjia ya kisayansi na kuyatumia baadaye watakapokuwa
tayari
0 comments:
Post a Comment