Ello
MTANDAO wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya
watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa
kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC
kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August
mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama
kulipia data.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la
Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa
mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda
mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya
Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na
kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.
Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala
bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao
wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment