NCHINI Tanzania hatimaye Serikali ya Tanzania hapo ilitoa vyeti vya uraia kwa waliokuwa wakimbizi wa zamani wa Burundi zaidi ya laki moja na elfu sitini na mbili ambao wamekuwa wakiishi kwa zaidi ya miaka arobaini kama wakimbizi, hatua inayoelezwa kuwa haijawahi kufanywa na nchi yoyote Duniani.
Sanjari na hatua hiyo Serikali ya Tanzania imesema hakutakuwa na mpango wa kuwahamisha kutoka katika makazi yao ambayo wamekuwa wakiishi kwa kipindi chote hicho na kwamba kwa sasa watakuwa huru kwenda kuishi popote kama raia wengine wa Tanzania ili mradi hawavunji sheria.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment