Jack Wilshere alionekana mwenye morali ya juu.
*******
JACK Wilshere na Danny Welbeck wameonekana kuwa na morali kubwa katika mazoezi ya Arsenal kujiandaa na mechi ya ligi ya mabingwa inayopigwa leo dhidi ya Borussia Dortmund.
Wilshere alifunga bao na kuonesha kiwango cha juu katika sare ya 2-2- na Manchester City, wakati Welbeck alifurahia kucheza mechi yake ya kwanza na kutolewa baadaye.Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alionekana kuimarika na katika mazoezi ya jana Arsene Wenger alikuwa anampa mazoezi ya kuongeza kasi.
Welbeck (katikati) alicheza dhidi ya Manchester ana ameonekana kuwa imara katika mazoezi ya Arsenal
Arsene Wenger akitoa maelekezo kwa wachezaji wake kuelekea mechi dhidi ya Dortmund itayopigwa leo huko Westfalenstadion
0 comments:
Post a Comment