![Agreed: Barcelona look to have beaten Manchester United to signing Thomas Vermaelen](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/08/08/1407488602333_wps_1_FILE_PHOTO_Arsene_Wenger_.jpg)
BARCELONA
imekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15 ili kuinasa saini
ya beki wa Asernal, Thomas Vermaelen, na taarifa hizi ni pigo kubwa kwa
mashetani wekundu, Manchester United waliotaka kumsajili.
Kilichobaki sasa ni makubaliani binafsi kati ya wakala wa Vermaelen na wakatalunya hao kabla ya kukamilika kwa dili hilo.
Jana jumatano, Barcelona walimtuma Raul Sanllehi kufanya makubaliano mjini London na wamefikia sehemu nzuri.
Wakatalunya
wametoa ofa ya miaka mitano, huku kukiwepo kipengele cha kuongezewa
mwaka mmoja zaidi na mshahara wa beki huyo utakuwa paundi elfu
themanini.
![New surroundings? Barcelona look set to sign Vermaelen on a four-year deal worth £80,000 a week](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/08/08/1407491441747_wps_6_BARCELONA_SPAIN_AUGUST_05.jpg)
Mazingira mapya? Barcelona wanaonekana kuelekea kumsajili Vermaelen kwa mkataba wa miaka minne na mshahara wa paundi elfu 80.
![Preference: Thomas Vermaelen is set to disappoint Barcelona and current club Arsenal by joining Man United](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/08/07/1407447532388_wps_1_LONDON_ENGLAND_MARCH_25_T.jpg)
Hakuna kwenda: Arsenal walitaka kumuuza Vermaelen Man United kwa kubadilishana na Chris Smalling.
0 comments:
Post a Comment