MWANAMUZIKI Diamond amefunguka kuhusu madai ya baadhi ya wasanii kuwa aliwaibia idea au nyimbo zao na kuzifanya zake.
Ameeleza kuwa malalamiko yao hayana ukweli kwa kuwa kuna maneno ambayo yamezoeleka na yanaweza kutumiwa na watu wote lakini anapoyatumia hutokea msanii aliyetumia maneno kama yale na kudai kuwa ameiba idea yake.
Ametoa mfano wa nyimbo kama Moyo Wangu ambao anasema baada ya kuimba wasanii wengine waliimba pia lakini hakuwahi kujitokeza kusema ameibiwa kwa sababu neno hilo linaweza kutumika na kila mtu kwa ufundi wake.
Diamond ameeleza pia kuhusu tuhuma za Wababa (ingawa hakumtaja jina) kuwa alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na sasa anauita Mdogomdogo.
“Sitaki niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna mtu anasema eti hii nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno la Kitorondo. Sasa mimi nikuadithie story fupi…mimi nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale, kuna bendi ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab nyimbo yao ya kwanza inaitwa Tandale (anaimba kidogo). Ukiacha hivyo, Kitorondo ni jina ambalo ni ngoma ambayo wanaimba hivyo (anaimba). Yaani hii ni nyimbo.
“Kuna msanii kaichukua kaiimba kama ilivyo ile nyimbo ya mdundiko. Halafu baada ya kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu akasema yeye kaibiwa nyimbo. Mimi nimepata taarifa nikasema ana akili kweli. Yeye ndio kaenda kuiba. Mimi nimetumia neno la Kitorondo kwa taaluma zangu za kimuziki naliingiza kwa namna gani kama neno, yeye anasema nimemuibia yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa kila sehemu nikienda nawaambia msiniulize maswali hayo kabisa.”
0 comments:
Post a Comment