Thursday, December 13, 2012

WANABLOG TUJIFUNZE KATIKA HILI


Mahakama ya Katiba Misri

Kutoka Misri
MAHAKAMA moja nchini Misri imempa mwanablogu mmoja kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa kukufuru na kudharau dini.

Alber Saber alikamatwa mwezi wa tisa baada ya majirani kumlaumu kwama ndiye aliweka kilinganishi cha mtandao kilichoashiria sinema iliyoidhihaki dini ya Kiisilamu, na iliyosababisha maadamano makali katika ulimwengu wa Kiislamu.
Bwana Saber, ambaye haamini Mungu yeyote na anayetoka familia ya Kikristo ya dhehebu la Coptic, anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iwapo atalipa dola 167 kama dhamana.

Kesi hii inazua maswala nyeti kuhusu uhuru wa maoni wakati raia wa Misri wakijiandaa kupiga kura ya maoni kuhusu katiba rasimu.

Wito Kutaka aachiliwe
Wanaharakati wa haki za banadamu wametoa wito kuwa Bwana Saber achiwe huru.

Kumekuwa na kesi kadhaa zinazohusiana kukufuru baadhi ya mambo nchini Misri katika miaka miwili tangu Hosni Mubarak apinduliwe, huku wengi wa washtakiwa ni wa dhehebu la Copts, ambao ni asilimia 10 ya idadi ya watu nchini humo

Ingawaje kumkufuru Mungu limekuwa kosa la jinai kwa miaka mingi, Kifungu 44 cha katiba rasimu kina kifungu maalum kinachopiga marufu kashfa dhidi ya manabii.
Chanzo: BBC

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI