Sunday, December 9, 2012

NIYONZIMA AONGEZA MKATABA WA MIAKA 2 YANGA KWA DOLA 70,000 NA MSHAHARA WA DOLA 3,000


Habari na Picha kwa hisani ya Shaffih Dauda
Zikiwa zimepita siku kadhaa za mazungumzo juu ya kuongezwa kwa muda wa mkataba kiungo mshambuliaji wa Dar Young African - Haruna Niyonzima, hatimaye siku ya jana klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati imefanikiwa kukubaliana kimsingi na mchezaji huyo kumuongezea mkataba mpya.

Taarifa rasmi nilizozipata ni kwamba Haruna Niyonzima ambaye amebakiza miezi sita katika mkataba wake na Yanga amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga.


"Niyonzima alikuja Tanzania siku tatu zilizopita kwa ajili ya mazungumzo na uongozi wa Yanga, lakini mwanzoni hawakupata muafaka, ila hatimaye jana alikubaliana na Yanga kuongeza mkataba wa miaka miwili kwa kulipwa dola 70,000 kama fedha ya usajili na mshahara wa dola 3,000 kwa mwezi," kilisema chanzo cha habari kilichokuwa karibu na uongozi wa Yanga.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI