Thursday, November 1, 2012

SHEIKH PONDA APANDISHWA KIZIMBANI, ANYIMWA DHAMANA

Sheikh Ponda Isa Ponda
Na Hilali Ruhundwa
Katibu mkuu wa Taasisi ya Jumuiya za kiislam Sheikh Ponda Isa Ponda pamoja na wenzake 49 wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Sheikh Ponda na wenzake wamefikishwa katika mahakama hiyo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, kujibu mashtaka yanayowakabili baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika

Katika mahakama hiyo, mshtakiwa namba moja ambaye ni Sheikh Ponda amezuiliwa dhamana yake kutokana na maslahi ya Jamhuri pamoja na usalama wa mtuhumiwa huku washtakiwa wengine wakikubaliwa kuwekewa dhamana kwa masharti ya mdhamini kuwa na kiasi cha sh. Milioni Moja pamoja na barua ya utambulisho.

Kwa upande wake wakili wa serikali Tumaini Kweka amesema kuwa ushahidi wa kesi hiyo unajitosheleza na kwamba watuhumiwa wanakabiliwa na mashtaka manne, ikiwemo Njama ya kutenda kosa kinyume na kanuni ya adhabu, ambapo mahakama itaanza kusikiliza kesi hiyo kuanzia Novemba 15 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI