Sunday, November 18, 2012

NICKI MINAJ AMUIGA MICHAEL JACKSON



MWANAMUZIKI Nick Minaj anaetamba kwa miondoko ya rap nchini marekani ameamua kufanya upasuaji na kubadili pua yake ilimradi tu kushepu muonekano wa sura yake.


Huku wengi wamekuwa wakijiuliza ni nini kinaendelea katika muonekano wa mwanadada huyo hasa linapokuja suala la ukubwa wa makalio yake, na ndipo mwanadada huyo miezi michache iliyopita akaweka bayana kuwa amekuwa akiongeza makalio yake ndio maana amekuwa akionekana na hips tofauti na kipindi hicho alivyokuwa anaanza kutokelezea katika ramani ya muziki.


Japo mwenyewe amekanusha kuwa hajafanya upasuaji, Nami nakupa fursa ya kuangalia picha hizi hapa chini ili ujaji mwenyewe...
Picha ya Kushoto ni Kabla ya uvumi huo na Picha ya kulia ni baada ya kusemekana amefanya upasuaji huo. (Picha: Celebrityplasticsurgery.tv)
PICHA NYINGINE ZA NICKI MINAJ
Nicki Minaj ambaye ni jaji mojawapo akiwa na Mariah Carey katika mashindano ya kusaka vipaji ya X-FACTORS .
Jopo la majaji wakiwa wamepozi kupata picha ya pamoja.
Hayo ndio ambayo Nicki Minaj hivi karibuni yamekuwa yakijili katika maisha yake. Licha ya yote hayo kutokea mwanadada huyo amekuwa ni mwanamuziki ambaye amewavutia wengi watamani kuwa kama yeye hasa watoto wa kike, ambapo katika video zinazotumwa kupitia mtandao wa YOU TUBE, watoto wawili Sophia Grace na Rosie walirekodi video yao ambayo waliimba nyimbo ya Nicki Minaj, ambayo ilitazamwa na watu wengi duniani akiwemo Nicki Minaj mwenyewe.

Nicki Minaj akasema baada ya kuiona video hiyo kwa muda wa dakika kama tano hivi, alijikuta anawapigia watu wengine ili waione, na watu wengine pia walimpigia kumwabia aangalie video hiyo.

Mwanamama ellen anayeendesha kipindi cha Televisheni cha Ellen show akaamua kuwakutanisha na Nicki Minaj katika show yake, ambapo walifurahi sana hadi Sophia Grace kusema yeye ni Nicki Minaj wa pili ''am second Nicki Minaj''

ITAZAME SHOW HIYO HAPA...

1 comments:

  1. haya sasa na hii wabongo igeni maana siku hizi hadi mna hereni kumikumi kila sehemu........samahani lakini........napita tu

    ReplyDelete

ZILIZOSOMWA ZAIDI