Wednesday, November 7, 2012

KIMATAIFA - IRAQ WATU 27 WAFARIKI, 40 WAJERUHIWA VIBAYA!


Gari lililokuwa limetegwa bomu
Na Aziza Gulu
Mlipuko uliotegwa kwenye gari imesababisa vifo vya watu 27 kuuwwa na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa ambao umetokea katika mji wa taji mashariki mwa Baghdad huku shambulio hilo likitajwa kumuhusu kijana mmoja ambaye alihudhuria siku ya jeshi katika nchi hiyo.
Baadhi ya watu wakiwatizama wenzao waliokumbwa na mlipuko huo
Imeelezwa kuwa wanajeshi 19 ni kati ya watu waliouwawa katika shambulio hilo ambalo lilitokea katika lango la jeshi kwa mujibu afisa wa matibabu pamoja na wa ulinzi

Shambulio hilo ni la pili kutokea katika mji wa Taji baada ya masaa 24 toka jumatatu ulipotokea mlipuko mwingine, ambapo mashumbilio kadhaa yamekuwa yakitokea kutokana na  baadhi ya vikundi ambavyo vinamahusiano na alquaida kupinga utawala wa raisi wa Iraq Jalal Talabani baada ya majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI