NI
shidaah! Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Ngoyai
Lowassa (pichani) kukaribishwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, mastaa mbalimbali Bongo wameamua na
wengine kushawishiwa kumfuata wakiamini katika uwezo wake kiuongozi.
Chanzo
makini kililieleza gazeti hili kwamba mastaa wote waliokuwa wakimuunga
mkono Lowassa wakati akiwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais na baadaye
jina lake kukatwa kabla ya kufikishwa Kamati Kuu (CC), wameamua kuhamia
Ukawa kumfuata mwanasiasa huyo aliyejiunga huko kupitia Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
TUJIUNGE NA CHANZO
“Moto
huku Ukawa umewaka. Yale makundi mawili ya M4C (Movement For Change-
Chadema) na 4 U Movement (Kundi la Marafiki wa Lowassa) sasa yameingia
kazini. Mkakati maalum umeandaliwa kuhakikisha kila mwenye ushawishi
katika jamii anafikiwa, wakiwemo wasanii wa sanaa mbalimbali.
“Wameanza
na wasanii waliokuwa nyuma ya Lowassa kwa sababu wanaamini wana wafuasi
wao, ambao watashawishiwa wawashawishi hao watu wao wawaunge mkono
katika kuhakikisha wanaing’oa CCM madarakani,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu.
WEMA AKARIBISHWA
Chanzo
hicho kimeweka wazi kuwa licha ya wasanii kwa jumla, lakini pia mastaa
wenye mvuto mkubwa kwa jamii watafuatwa wao rasmi, kama ilivyotokea
majuzi ambapo mwigizaji Wema Isaac Sepetu alifuatwa na 4 U Movement
(Team Lowassa) kushawishiwa kujiunga na Team Lowassa.
Wiki
iliyopita Wema alitoswa katika kura za maoni za kuwania Ubunge wa Viti
Maalum (UWT-CCM) Mkoa wa Singida kwa kushika nafasi ya nne, lakini
akapokewa kwa kishindo katika mapokezi yaliyojaza watu jijini Dar.
“Yaani
Wema hivi karibuni aliitwa na watu wa Lowassa kwenye hoteli moja
maarufu jijini Dar ambapo ajenda kubwa ni yeye kuungana na Ukawa kwa
vile wanaamini ana mashabiki wengi,” kilisema chanzo hicho.
HUYU HAPA WEMA
“Ni
kweli, juzi nilipigiwa simu na watu waliojitambulisha kuwa ni Team
Lowassa, wakasema wana mazungumzo na mimi, ilikuwa tukutane Jumanne,
lakini nilikuwa na shughuli nyingine nikashindwa kwenda.
“Tulikubaliana
tukutane jana, lakini sijaelewa hasa ajenda ni nini na kwa maana hiyo
siwezi kusema lolote kwa sasa kama ninaenda Ukawa au la,” alisema
muigizaji huyo, alipozungumza na gazeti hili.
Jacquiline Wolper.
WOLPER ACHOCHEA
Kana
kwamba haitoshi, staa mwingine wa filamu za Kibongo, Jacqueline Walper
Massawe ambaye tangu awali alijitoa muhanga kufa pamoja kisiasa na
mbunge huyo wa Monduli, anatajwa kuwa kinara wa kampeni katika mitandao
mbalimbali ya kijamii akiweka wazi kuwa atamfuata Lowassa popote
atakapokwenda kwani ni shabiki wake mkubwa.
Aunt Lulu.
AUNTY LULU RASMI UKAWA
Ahadi
kama hiyo ilitolewa pia na mwanadada Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’
aliyetangaza kujiunga rasmi na Ukawa kwa sababu ya Lowassa.
Kala Jeremiah.
Mastaa
wengine ambao wamemfuata Lowassa Ukawa ni pamoja na Deogratius Shija,
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Kala Jeremiah, Khalid Ramadhan
‘Tunda Man’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na
Bahati Bukuku.
0 comments:
Post a Comment