Wednesday, September 23, 2015

NIMEKUMISS’ YA MWANAMKE, ‘NIMEKUMISS’ YA MWANAUME, TOFAUTI


Tunakutana katika mada hii ya maisha na mapenzi. Ni somo ambalo litaweza kukusaidia katika kubadilika hususan kama wewe ni mwanandoa au upo katika uhusiano!
Leo katika makala haya nazungumzia neno maalum kabisa katika uhusiano linaloitwa miss! Miss yaani kosa, pia ‘kosana’ hutumiwa zaidi na watu wenye uhusiano wowote ule, iwe ndugu, wapenzi na hata marafiki walioshibana.

MATUMIZI YAKE
Ni neno la Kiingereza ambapo watumiaji wanapaswa kuwa Waingereza wenyewe lakini pia wasio Waingereza ambao wanajua maana yake.
Hutumika kwa watu waliopotezana kwa muda ambao mhusika amehisi kumkumbuka mwenzake kwa maana ya kuonana naye laivu.
“Shoga, upo?”
“Nipo shoga yangu, niambie, mzima?”
“Mi mzima tu, nimekumisi ‘miss’ ile mbaya.”
“Nimekumisi pia shoga yangu.”
Maneno hayo ni watu wawili walioshibana ambapo wamepotezana au hawajaonana kwa siku kadhaa. Idadi ya siku za ‘kumisiana’ hutegemea mtu na mtu na si kwamba ni kiwango cha kimataifa kuwa lazima ziwe siku mia moja!

MATUMIZI MENGINE
Matumizi mengine ya neno hili limekuja kujikita kwa watu walio kwenye uhusiano wa kimapenzi. Walio wengi wanapokuwa kwenye mapenzi, hufika wakati kila mmoja akatamani kuwa na mwenzake ‘laivu’ kwa maana ya kukaa pamoja na kuzungumza au kuonana tu pia kunashibisha hamu ya upendo.
Wapenzi walio wengi, iwe mke na mume au wachumba na hata wasiokuwa na vyeo vyote viwili hulitumia neno kumisi kama ishara ya kukumbukana kwa maana kuonana laivu.

MFANO MZURI NI HUU
Mfano mzuri, wapenzi wawili, mmoja amesafiri hivyo kuwa mbali na mwenzake, sasa yeyote yule anaweza kumkosa mwenzake kama ilivyo mazoea yao. Hivyo ni rahisi kumsikia mmoja akianza:
“Baby nimekumisi sana.”
“Hata mimi nimekumisi pia mpenzi wangu.”
“Unarudi lini baby?”
“Wiki ijayo baada ya kumaliza hii kazi.”
“Poa baby, nakutakia kila la kheri.”
“Asante baby.”
Hawa wawili wamemisiana kwa kutoonana laivu kutokana na mmoja kuwa mbali na mwenzake tofauti na mazoea yao.

LAKINI SASA
Pamoja na yote hayo, uchunguzi wa kawaida nilioufanya nimebaini kuwa, neno nimekumisi limekwenda mbele zaidi na kutumika katika uhitaji wa tendo la ndoa, hasa kwa wanawake!
Kivipi? Wapenzi, baadhi yao tena kwa sehemu kubwa wamekuwa wakilitumia neno hili kwa maana ya kutaka kukutana kwa tendo la ndoa.
Unaweza ukakuta wapenzi wanaishi mbalimbali, wamekutana asubuhi lakini jioni, mmoja anamtumia meseji mwenzake ya kumwambia amemmisi sana.
Nilijaribu kutafuta maana yake nini, je ni kumisi kwa maana ya kumuona laivu nikajua si hivyo, nimekumisi hii ni ya kutaka kukutana kwa tendo la ndoa.

TOFAUTI YA MWANAMKE NA MWANAUME!
Ila sasa, kuna tofauti kubwa ya misi ya mwanamke na misi ya mwanaume! Katika wanawake kumi, nane hulitumia neno hili kwa maana ya kutaka kukutana kwa tendo la ndoa tofauti na misi ya mwanaume ambao karibu wote hulitumia kwa kutaka kuonana laivu.
Kama wewe ni mwanaume, una mpenzi wako, tena mkeo kabisa, mko nyumba moja, kitanda kimoja, unaweza kuwa kazini akakutumia meseji kukwambia amekumisi lakini yenye maana ya tendo la ndoa.
Kama wewe ni mwanamke, una mpenzi wako, ni mumeo, ukiwa mbali naye kwa siku nzima, anaweza kukutumia meseji ya hivyo akimaanisha kutokukuona laivu.

WAPENZI, WACHUMBA
Kundi hili ndilo linathibitisha matumizi hayo. Kwamba, wapenzi, wachumba wanaweza kukutana saa kumi jioni, wakiachana usiku, msichana akatuma meseji ya misi akimaanisha kukutana kimwili.
Mara nyingi sana, wanawake hulitumia neno hilo kwa maana hiyo. Nimefanya utafiti na kubaini hilo. Hata wapenzi wanapokuwa hawajakutana kimwili kwa siku kibao, mwanamke akijisikia anakuwa mgumu sana kusema wazi kwamba anahitaji tendo hilo, njia yake kubwa ni kusema ‘baby nimekumisi’ wakati mwanaume huenda moja kwa moja.
Kwa hiyo nathibitisha kwamba, nimekumisi ya mwanamke na nimekumisi ya mwanaume tofauti! Hivyo wanaume mnapaswa kulijua hilo badala ya kudhani ni ile ya kutokuonana na wewe ukajibu ‘na mimi pia’.
Tukutane wiki ijayo katika mada nyingine.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI