MGOMBEA urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataunda serikali itakayokuwa na viongozi wenye uwezo wa kuchukua hatua na kutatua matatizo ya wananchi na atahakikisha utaratibu wa wananchi kulalamika na viongozi pia kulalamikakama ilivyo sasa unabaki kuwa historia.
Mh Lowassa ambaye amefanya mikutano minne katika majimbo ya Mtera, Bahi Chilonwa na Dodoma mjini pia amewaomba watanzania kumpa nafasi ya kukamilisha ndoto yake ya kuleta usawa wa huduma za kijamii ikiwemo elimu aliyoanza kuonyesha mfano kupitia shule za kata alipokuwa waziri mkuu.
Nao Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye na mwanasheria wa Chadema Mh Tundu Lisu wakihutubia juzi mjini Dodoma walisema kukithiri kwa malalamiko ya wananchi kukosa huduma huku wanaotakiwa kuchukua hatua wakiendelea kutoa ahadi inatosha kuonyesha kuwa uwezo wao wa kupata ufumbuzi umefika mwisho na ndio maana UKAWA inaomba nafasi ya kuondoa tatizo hilo.
Wananchi na viongozi wa jimbo la Mtera walisema ubinafisi wa viongozi wa CCM, na ahadi zisizotekelezeka umesababisha wapoteze matumaini ya kuondokana na umaskini hasa kwa vijana.
Akihitimisha mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Dodoma uliofanyika Dodoma mjini, Mh Lowaasa ambaye sasa yupo mkoa wa Singida aliendelea kunadi sera za UKAWA na kutoa ufafanuzi wa namna ya kuzitekeleza kwa wakati na kwakasi inayostahili.
0 comments:
Post a Comment