Sunday, June 28, 2015

IDADI YA WALIOUAWA HOTELINI TUNISIA YAZIDI KUONGEZEKA

 
Waliouawa na wakitolewa eneo la ufukweni.
 
Eneo la ufukwe ambapo shambulio hilo lilitekelezwa.
 
Waliouawa, miili yao ikiwa imefunikwa.
 
Mmoja kati ya waliotekeleza shambulio hilo akipewa kipigo baada ya kukamatwa na Maofisa wa Ulinzi wa Tunisia.
 
Maofisa wa Ulinzi wakiimarisha ulinza eneo la tukio.
 
Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi akimsalimia mmoja kati ya majeruhi wa shambulio hilo.
Sousse, Tunisia
Kutokana na shambulizi la wenye silaha katika hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye Ufukwe wa Pwani ya Tunisia jana, idadi ya watu waliokufa imefikia 38 mpaka sasa huku wengine 36 wakiwa majeruhi.
Maofisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na Maofisa wa ulinzi wa nchi hiyo na kuwa waliosalia bado wanasakwa na Jeshi la Polisi.
Kundi la wapiganaji wa ISIS wamethibitisha kutekeleza shambulio hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika Mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka Bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.
Waziri Mkuu wa Tunisia, Habib Essid amesema kuwa, miongoni mwa watalii hao wengi wao walikuwa ni raia wa Uingereza, na wengine wanatoka Ujerumani, Ubelgiji na nchi nyingine.
Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli za watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni kuanza kuwamiminia risasi mpaka kusababisha mauti watalii hao.
Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunisia.
October 2013, Mlipuaji wa kujitoa mhanga, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya Maofisa wa Polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia.
CHANZO BBC NA DAILY MAIL

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI