Tuesday, January 6, 2015

WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA JIJINI ARUSHA WAPEWA CHANGAMOTO

Na Mwandishi wetu
WENYEVITI wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, wametakiwa kuwahudumia wananchi waliowachagua bila ubaguzi wa itikadi za vyama vyao.
Rai hiyo ilitolewa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa Jiji la
Arusha,Juma Idd wakati alipokuwa afungua semina elekezi ya siku moja kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa 154,waliochaguliwa Disemba 14, Mwaka jana.
Alisema kuwa wakati wa kampeni pamoja na uchaguzi umeisha hivyo viongozi hao wana wajibu wa kuwajibika kwa wananchi waliowachagua bila kujali itikadi za vyama vyao.
“Ninawaomba sana muweke itikadi za vyama pembeni, wajibikeni kwa wananchi waliowachagua,tambueni kuwa wananchi waa matarajio makubwa katika kuwatatua changamoto zinazowakabili”alisema Idd
Akizungumzia chnagamoto la baadhi ya mitaa kutokuwa na Ofisi, Mkurugenzi huyo alisema kuwa Halmashauri hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa ofisi kwa ajili ya wenyeviti hao wa Serikali za mtaa.
“Katika Jiji letu tunakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa ofisi za wenyeiviti wa vijiji ila naagiza kwa sasa ilipo Ofisi ya Mtendaji wa kata na ofisi ya Mtaa iwe hapo hapo,tatizo hilo tutalishughulikia ila tunapaswa kushirikiana kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kutafuta maeneo ya kujengwa kwa ofisi”alisema Mkurugenzi
huyo
Aidha aliwatahadharisha baadhi ya viongozi wenye tabia ya matumizi mabya ya mihuri ya ofisi,na kusema kuwa Halmashauri itasimamia matumizi sahihi ya mihuri hiyo kwani katika kipindi cha nyuma kulikuwa na matumizi mabaya ya mihuri.
Wakichangia katika semina hiyo,wenyeviti hao walilalamikia tatizo la ukosefu kwa ofisi kwa ajili yao,jambo linalowafanya wengi wao kutembea na mihuri mifukoni.
Waliuomba uongozi wa  Halmashauri hiyo kuzunguka katika kata zote 25 na kuona namna ya kujenga ofisi katika maeneo yasiyo na ofisi.
Aidha semina hiyo elekezi pia iliwashirikisha Watendaji wa Kata zote 25 za Jiji hilo,wakuu wa Idara,ambayo ilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na kuwaelemisha viongozi hao juu ya usimamizi na uendeshaji wa mikutano,viongozi wanaotarajiwa kuapishwa kuanzia Januari 6, Mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI