Saturday, January 31, 2015

MMMH…JOJO KIDOTI + MILLARD AYO KUNAKO KEKI YAKAIBUKA MAMBO MAZITO! FUATILIA HAPA!

‘Mtu wa Nguvu’ Millard Ayo na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakifurahia jambo kwenye ‘bethidei’ yake. Stori: Hamida Hassan na Musa Mateja/Ijumaa 
Keki iliyoandaliwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa ajili ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Millard Ayo ‘Mtu wa Nguvu’ imeibua mambo kwa mashabiki wao. 
Ishu hiyo ilijiri Januari 26, mwaka huu ambapo Jokate alidaiwa kuangusha pati nyumbani kwa jamaa huyo maeneo ya Ubungo-Msewe jijini Dar. 
Kwenye pati hiyo, Millard ambaye ni mtangazaji mkali wa Vipindi vya Amplifaya na Top 20 vya Clouds FM, alidaiwa kumwalika Jokate ambaye mashabiki wao walimpa jina la Special Girl (msichana maalum). 
Pia katika pati hiyo, ‘ubuyu’ ulienea kwamba Jokate ndiye aliyekaangariza madikodiko na kupakua nyumbani kwa jamaa huyo kisha akamwandalia bonge la keki

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI