Saturday, January 31, 2015

MEYA WA MORO, DEREVA NA MWANDISHI WAKIMBIZWA MUHIMBILI KWA MATIBABU

MSTAHIKI Meya wa halmashauri ya manispaa  ya Morogoro, Amir Nondo (45), Dereva  Mwambala Ally (55),  na Mwandishi wa habari ambaye ni mpiga picha wa Televisheni, Hussein Nuha (28) ,wamehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kwa uchunguzi wa kina na kupatiwa matibabu zaidi.
Hayo yamesemwa leo na Mganga mkuu wa mkoawa Morogoro , Godfrey Mtei , akielezea hali ya majeruhi hao ambao waliokuwa wamelezwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya  kujeruhiwa wakati gari lao lilipogongwa na basi la abiria lenye namba za usajili T 831 CEH, aina ya Scania mali ya kampuni ya Happy Africa likitokea mkoani Njombe.
Tukio hilo lilitokea Januari 30, mwaka huu majira ya saa 9: 30 alasiri , eneo la Msamvu Mzambarauni darajani katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam, ambapo basi hilo lilikuwa likotokea mkoani Njombe.
Hata hivyo alisema, mwandishi mmoja, Anitha Chali (30)  ambaye amelezwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro anaendelea vizuri na wakati wowote anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI