KIONGOZI mmoja wa dini ambaye alipata
umaarufu nchini Kenya kwa kutabiri mwisho wa dunia mwaka 2006 amezikwa
katika kijiji cha Bomet.
Kiongozi huyo wa madhehebu ya House of Yahweh Willy Kiplangat Sang alizikwa masaa machache baada ya kifo
chake katika shamba la babaake kijijini Matarmat katika sherehe iliohudhuriwa na jamii yake ,majirani na wafuasi wa kanisa hilo.
Ndugu za nabii huyo aliyezingirwa na utata
wanasema aliugua ugonjwa wa kifua kikuu nyumbani mwake huko Mauche
kaunti ya Nakuru ambapo alikuwa mkulima na muhubiri.
0 comments:
Post a Comment