MENGI yameibuka kufuatia waimba Injili Bongo kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo ndoa zao kuvunjika, madai ya kuchepuka, kupata ujauzito nje ya ndoa na matumizi ya madawa ya kulevya, Uwazi limechimba na kuchimbua.
Janet Mreme akiwa na mume wake Jonas Mrema.
BADO JINAMIZI LA KUVUNJA NDOA LAWAANDAMA.
Mpaka sasa, waimba Injili wanawake wameshakumbwa na mikasa mbalimbali lakini mpya kabisa ni madai ya hivi karibuni kwamba, ndoa ya mwimbaji mwingine, Kabula George imesambaratika.
Kabula George mwaka 2012 alitamba na Albamu ya Nitang’ara Tu! Inadaiwa hayuko kwa mumewe baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka nane!
JANET MREMA ANAUMWA
Huyu aliwahi kuripotiwa na Gazeti la Amani miezi miwili iliyopita kwamba, ndoa yake na mumewe, Jonas Mrema imesambaratika madai makubwa ni mume kutomwamini mkewe huyo na kudai alitoroshwa nyumbani na mchungaji mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyejulikana kwa jina moja la Emmanuel.
Habari mpya ni kwamba kwa sasa hali yake ni tete, anaumwa lakini wengi wanaamini ugonjwa wake unatokana na mawazo ya kuchanika kwa ndoa yake.Tayari mwanaume huyo ameshafungua kesi Mahakama ya Kinondoni, Dar akimlalamikia Mchungaji Emmanuel kumtoroshea mkewe. Anataka fidia ya pesa ambazo mahakama itaamua kama itaona ni sahihi.Bahati Bukuku.
BAHATI BUKUKU
Huyu ni mwimba Injili mkongwe Bongo. Ndoa yake na Daniel Basila ilivunjika mwaka 2005, mume alimtuhumu Bahati kutoroshwa nyumbani na mzungu mmoja ambaye hakumtaja jina.
Baadaye Bahati alikanusha, akasema aliamua kuondoka nyumbani kwa Daniel kutokana na manyanyaso mengi. Alishindwa kuvumilia. Mpaka sasa, Bahati hayuko kwenye ndoa.
Rose Mhando.
NEEMA MWAIPOPO
Alipovuma sana na wimbo wa Sipati Picha alikuwa akijulikana kwa jina la Neema Mushi. Mumewe ndiye Mushi. Baadaye, ndoa yake ilivunjika, akarudia jina la ukoo wake, Mwaipopo. Akatoa albamu inaitwa Raha Jipe Mwenyewe.
ROSE MHANDO
Rose Mhando ndiyo anavyojulikana na wengi. Jina la baba yake ni Athuman. Familia yake yote ni ya Kiislam.
Majanga yake makubwa ni kuzaa watoto watatu pasipokuwa na ndoa. Lakini kwa sasa ana mimba tena, ina maana ni ya mtoto wa nne! Ilishawahi kuandikwa kuwa, kila mtoto ana baba yake!
Lakini pia, Rose aliwahi kudaiwa kubwia ‘unga’ hali inayosemekana kumpotezea utendaji wa huduma.
FLORA MBASHAFlora Mbasha.
Huduma yake kwa sasa ni kama imesimama baada ya ndoa yake na mumewe, Emmanuel Mbasha kuparaganyika!Kwa sasa, Flora yuko mahakamani akimdai talaka mumewe huyo kwa madai kwamba, kwa kipindi chote cha ndoa yao, alikuwa mtu wa kupigwa mara kwa mara!
CHRISTINA SHUSHO!
Na yeye ni mwimba Injili maarufu. Kwa miaka ya hivi karibuni ni kama amezimika! Ilidaiwa naye ndoa yake ina misukosuko ya mara kwa mara. Uwazi liliwahi kumfuata nyumbani kwake, Tabata-Chang’ombe, Dar ili kuujua ukweli wa ndoa yake kukumbwa na upepo wa kisulisuli, msichana wa kazi aliyefungua geti alisema:
“Dada yupo kwenye kikao cha usuluhishi, kuna mchungaji kaja.”
Christina Shusho.
SARAH MVUNGI
Ni muimba Injili aliyetokea kwenye fani ya maigizo. ana watoto wawili, kila mmoja ana baba yake. Hana ndoa lakini anatoa huduma ya Neno la Mungu kwa njia ya uimbaji.
JENNIFER MGENDI
Huyu kidogo Uwazi limepekua maisha yake na kubaini kwamba, yemejaa uadilifu. Ndoa yake haikuwahi kudaiwa kukumbwa na kimbunga cha kusambaratika wala kutengana.
Jennifer Mgendi.
MCHUNGAJI ATOA NENO
Mchungaji mmoja wa Kanisa la Evangelical Asemblies of God Tanzania (EAGT) ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema:“Nawaomba hao waimbaji wa kike, hasa wanaodai talaka au walioshindwa kuvumilia maisha ya kwenye ndoa wasome maandiko, mbona yako wazi sana.
“Mimi natabiri kwamba, muziki wa Injili unaporomoka na utazidi kuporomoka kwani shetani amefanikiwa kuwashika waimbaji kwa kusambaratisha ndoa zao kwanza ili washindwe kutoa huduma ya kiroho, maana utahubirije Neno la Mungu wakati wewe linakushinda kulitekeleza?”
KUNA NINI KWENYE INJILI?
Ni swali la kujiuliza sana, ni kwa nini maisha ya waimba Injili, hususan wanawake yako hivi? Mtu anayetoa huduma ya kiroho anapofikia hatua ya kusema ‘ameshindwa kuvumilia’ inakuaje kwa asiyejua maandiko?
Chanzo: UWAZI/GPL
0 comments:
Post a Comment