Tuesday, November 18, 2014

UKATILI HUU UTAISHA LINI?: MWANAMKE ANUSURIKA KIFO KISA VOCHA YA SIMU

MWANAMKE mmoja amenusurika kuuwawa kutokana na kupigwa na mume wake ambaye ni askari, kisa ikiwa ni mwanamke huyo kushindwa kumnunulia vocha.
Akisimulia mkasa huo uliotokea Uganda, mke wa askari huyo Eva Okoth anasema mume wake alikuwa ametoka kunywa pombe na rafiki zake, akaanza kujisikia vibaya baada ya kushindwa kula na kutapika akihisi rafiki zake walimwekea sumu katika pombe, hivyo akampatia hela mke wake ili akanunue vocha kuwapigia ndugu zake ili awaage kwamba anakufa.
Mwanamke huyo anasema wakati huo ilikuwa saa 11 alfajiri, maduka yalikuwa hayajafunguliwa, askari huyo alichukua bunduki na kuanza kufyatua risasi huku akitishia kumuua na kujiua yeye.

Eva alikimbia kujificha jikoni, taarifa kutoka kwa msemaji wa kituo cha Polisi Lameck Kigozi amemtambua askari huyo kuwa ni John Okoth.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI