Monday, November 10, 2014

SAFARI YA MWISHO YA MWANAMUZIKI AMIGOLAS KATIKA MAKABURI YA KISUTU, DAR ES SALAAM! *PICHAZ*

Mwili wa marehemu, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ ukiwasili nyumbani kwao Mburahati leo jijini Dar es Salam.
Mjane wa marehemu, Bi Modesta Emmanuel akiwa amezimia msibani.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere 'Steve Nyerere'akiwasili msibani.
Mkurugegenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa msibani.
Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakilia msibani.
Mwili wa marehemu, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ ukibebwa na waombolezaji kuelekea katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Filamu nchini, Jacob Steven 'JB' (wa pili kutoka kulia) akielekeamakaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Waombolezaji wengine wakijiandaa kuelekea katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.MAZIKO ya mwanamuziki wa zamani wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ aliyefariki juzi amezikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na mamia ya watu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI