MAHAKAMA
ya Somalia imetoa amri ya kuzuiwa kwa pasipoti ya mmiliki wa kituo
maarufu cha redio nchini humo, ambaye anakabiliwa na shtaka la
kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.
BBC inaripoti
kuwa Abdimalik Yusuph mmiliki wa kituo cha redio Shabelle, ambaye ni
raia wa Uingereza aliachiliwa kwa dhamana na kuamriwa kukabidhi pasipoti
yake mahakamani kama dhamana, huku mwandishi mwingine akiendelea
kushikiliwa na jeshi la polisi.
Waandishi
hao ni miongoni mwa waandishi wa habari 4 wanaoshikiliwa na jeshi la
polisi nchini Somalia wakikabiliwa na shitaka hilo baada ya kuripoti
kuhusu mkakati wa Serikali ya nchi hiyo wa kuwapokonya silaha watu mjini
Mogadishu.
Nchi ya Somalia inatajwa kuwa ni moja ya nchi yenye mazingira hatari zaidi kwa waandishi wa habari.
Waandishi
wa habari wamelaani kitendo cha wenzao kushikiliwa na jeshi la polisi
kwa zaidi ya miezi 3 bila ya kufunguliwa mashtaka, kinyume na katiba ya
nchi hiyo.
Mahakama nchini humo imeahirisha kusikilizwa kwa kesi hiyo mpaka baada ya wiki mbili.
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment