Rose Mhando
MWANAMUZIKI mkali wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amedaiwa tena kuhusika katika utapeli wa shilingi milioni mbili.
Mwanamuziki
wa nyimbo za Injili, Rose Muhando. Muandaaji wa shoo hiyo, Ibrahim
alidai kuwa Rose alitumiwa kiasi hicho cha pesa kama sehemu ya malipo ya
kazi hiyo iliyokuwa ifanyike Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli
ya Landmark uliopo Ubungo, jijini Dar lakini hakutokea.
“Huu ni
utapeli wa hali ya juu, maana alipewa pesa yote ya shoo, cha kushangaza
hakutoa taarifa yoyote ya dharura, simu akipigiwa hapokei na wala meseji
hajibu,” alisema Ibrahim.
Rose
alipopigiwa simu ili kujua madai hayo kama yana ukweli, simu yake iliita
bila ya kupokelewa hivyo akatumiwa meseji ambayo nayo ilionesha
kumfikia lakini hakujibu chochote.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu.
Hivi
karibuni, Rose alidaiwa kuingia mitini na shilingi milioni moja
aliyopewa kama malipo ya kutumbuiza katika uzinduzi wa albamu ya
mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu.
0 comments:
Post a Comment