MCHUNGAJI
anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
(DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel amejikuta ndani ya majanga
kufuatia madai mazito kwamba amemtorosha mke wa mtu ambaye ni mwimbaji
wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema.
Mwimbaji
wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa
kutoroshwa na mchungaji huyo. Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji
huyo alifika nyumbani kwa Jonas Mrema, mume wa Janet, maeneo ya
Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na kuishi kama mtumishi wa Mungu lakini
polepole alianza mazoea tata na Janet.
“Mume
alianza kuhisi mabadiliko ya mkewe kwa mtumishi huyo, lakini nadhani
aliona ni mawazo yake tu. Ndipo siku ya siku akashangaa mkewe na
mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo.
“Kwa sasa
tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume alihangaika sana
kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo akampata wakiwa na
mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa wakiishi pamoja,”
kilisema chanzo chetu.
Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel akilizungumzia sakata hilo.
Iliidaiwa
kwamba, mchungaji huyo alipopekuliwa alikutwa na paspoti ya nchini
Burundi wakati yeye ni Mkongo wa Uvira na alionekana kuishi nchini
kinyume na sheria hivyo alifunguliwa jalada la kesi kwenye Kituo cha
Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu Na. WH/RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI.
Juzi,
Amani liliwasiliana na Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela
Joel ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari chama hicho
kimemsimamisha uanachana Janet kwa kitendo chake hicho cha kumtoroka
mumewe wa ndoa.
“Ni kweli
na Chama cha Waimba Injili Tanzania kimemsimamisha uanachama Janet.
Hatuna mzaha katika maadili,” alisema Stela.Amani lilimpigia simu mume
wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo baada ya salamu alipewa
pole kwa matatizo ya mkewe, alisema asante kisha alipoulizwa kuhusu hali
ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile alikuwa kikaoni.
Hata
hivyo, baada ya saa mbili kupita bila kupiga, Amani lilimpigia tena simu
ambapo iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment