Sunday, October 19, 2014

KITUKO CHA MWAKA: DEREVA ASHUSHA KIPIGO KWA KIBAKA BALAA. *VIDEO*


KATIKA kituko hiki kilichotokea katika jiji la ConcepciĆ³n, nchini Chile, huyu kibaka, alipodaiwa nauli mara baada ya kuingia kwenye basi, alimwambia dereva kuwa hana nauli, na kuwa mmoja wa abiria ni shangazi yake (kitu ambacho si kweli.) Kisha akaanza kutoa visingizio kibao, akisubiri nafasi ya kukwapua pochi. 


Dakika ya mwisho, wakati basi linaanza kufunga mlango, alijaribu kukwapua mkoba wa mwanamke aliyekaa siti ya mbele. Bahati nzuri alishindwa kuiba mkoba huo, halafu alichelewa kutoka nje ya basi na kunaswa na mlango uliokuwa unajifunga. Hapo ndipo dereva alipotoa rungu lake na kuanza kumpa kichapo huku akiendelea kuendesha basi. 



Kibaka huyo aliendelea kula kichapo huku akijitetea au kuomba msamaha, mpaka basi liliposimama mbele ya askari polisi, na askari huyo kumtia mbaroni. Taarifa zaidi zinasema kuwa kibaka huyo ana historia ya uhalifu, na kwa sheria za nchi hiyo, ambazo ni kali kwa wahalifu wanaorudia makosa, ataishia jela.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI