Facebook imewachukulia hatua wanaouza Likes kwenye Facebook.
MTANDAO wa kijamii wa
Facebook umeahidi kujitahidi kukabiliana na uuzaji na ununuzi wa 'Likes' bandia
kwenye mtandao huo.
Facebook inasema
imeshinda dola bilioni mbili katika kesi iliyowasilisha mahakamani dhidi ya
watu wanaouza 'Likes' za bandia kwa wafanyabiashara walio na akaunti kwenye
mtandao huo.
Inaarifiwa wamiliki
wa makampuni wananunua 'Likes' kwenye mtandao huo ili akuanti zao kuonekana
kuwa maarufu na kupendwa na watu wengine wakati sio kweli.
Lakini Facebook
imesema kuwa wanunuzi wa 'Likes' kwa njia za kimagendo wanafanya jambo baya kwa
wafanyabiashara wengine na ina maana kuwa kampuni nyinginezo zenye akaunti zao
kwa Facebook heunda zikapata hasara.
Katika taarifa yake,
Facebook iliandika na kusema: 'Tunataka kuhakikisha tunakomesha tabia ya
ununzzi wa 'Likes' kwa sababu wenye biashara na watu wa kawaida wanataka
kuwasiliana kwa lengo la kupata mafanikio sio mambo bandia. ''
Mtandao huo ulielezea
kuwa wauzaji wa Likes bandia wanawapa 'admins' au wasimamizi wa akaunti fulani
fursa ya kununua 'Likes' kama 10,000 bandia ili watu wapende akaunti zao.
Kwa sababu sakata
kama hizi zinalenga zaidi kufaidika kifedha na hasa kuwahadaa wafanyabiashara ,
tunalenga kuwakomesha watu kama hao.
Mtandao huo umesema
mbali na kuchukua hatua za kisheria pia unalenga kutumia teknolojia mpya ya
kubana uuzaji na utengezaji wa Likes bandia.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment