Mkuu
wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Bw.
Comfort Komba akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) Kuhusu
mafanikio yaliyofikiwa na Ofisi hiyo ikiwamo ujenzi wa majengo ya chuo
cha ukutubi na uhifadhi wa nyaraka kilichopo Bagamoyo na uzinduzi wa
maktaba za wilaya za Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na
Mbulu, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi. Georgina Misama.
Na Hassan Silayo-MAELEZO.
BODI ya Huduma za Maktaba Tanzania
imeanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi katika Kampasi ya Dar
es Salaam katika mwaka wa masomo 2014/2015.Hatua hiyo inatokana na
kuongezeka kwa maombi ya wanafunzi wanaohitaji kuendelea na masomo baada
ya kuhitimu mafunzo ya cheti.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za
Maktaba Tanzania Bw. Comfort Komba wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam. Comfort alisema kuwa masomo hayo kwa
awali yalikuwa yakitolewa katika kampasi ya Bagamoyo lakini kutokana na
kuongezeka kwa uhitaji wa masomo hayo ambapo mpaka sasa kuna wanafunzi
wapya 130.
“Bodi ya
Huduma za Maktaba Tanzania imeamua kuanzisha masomo ya jioni ya diploma
ya ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo
2014/2015 na utaratibu huu tunautekeleza kutokana na kuwepo kwa ongezeko
la uhitaji wa wanafunzi” Alisema Comfort.
Aidha
Comfort alisema kuwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania kwa kushirikiana
na halmashauri za Wilaya na Mikoa imefanikiwa kuanzisha maktaba katika
wilaya mbalimbali ikiwemo Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge,
Masasi na Mbulu.
Akizungumzia
kuhusu uhufadhi wa machapisho ya kitaifa, Comfort alisema kuwa Ofisi
hiyo imefanikiwa kuhifadhi jumla ya vitabu 1,300,000 pamoja na majarida
950,000 tangu Bodi hiyo ilipoanzishwa katika ngazi ya Mikoa, Wilaya hadi
Tarafa.
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ni Shirika la umma lililopo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
0 comments:
Post a Comment